Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (wa pili kushoto) akipiga krosi huku akizongwa na mabeki watatu wa Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam,jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ramadhan Shiza Kichuya katika dakika ya 57 na dakika tatu baadaye Yanga wakasawazisha kupitia kwa Obrey Chirwa dakika ya 60. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Chirwa akitulia mpira gambani huku beki wa Simba akijiandaa kumkabili.
Beki wa Simba Mohamed Hussein akiokoa mpira wa kichwa
Kikosi cha Yanga, kilichoanza
Kikosi cha Simba kilichoanza

Huyu babu inaelezwa kuwa yupo katika Benchi la Ufundi la Simba, lakini cha ajabu amekuwa akikamatwa uwanjani katika baadhi ya mechi akisadikiwa kufanya ushirikina. Hapa akitolewa uwanjani baada ya kuoneka akiwa nyuma ya goli la Kaskazini wakati wachezaji wa timu yake wakipasha misuli moto.
Akisindikizwa kuondolewa nyuma ya goli
Akiwataka walinzi kumpeleka kwenye benchi la Simba
Kabla ya mchezo huo timu za Vija za Yanga na Simba zilicheza mchezo wa utangulizi, pichani ni Winga mwenye mbio wa Yanga U20, 'Boxer' akiruka kupiga mpira 'kidhungu' na kuukosa akitafuta bao la pili. Katika mchezo huo Yanga walishinda bao 1-0.

Ajib (kulia) akiwania mpira na Muzamiru wakati wa mchezo huo.
Geofrey Mwashiuya (kulia) akiwania mpira na Haruna Niyonzima
Chirwa (kushoto) akimiliki mpira huku akizongwa na Niyonzima
Hekaheka langoni mwa Simba
Kichuya (kushoto) akijaribu kumhadaa beki wa Yanga Gadiel Michael.
Ibrahim Ajib (katikati) akiwatoka mabeki wa Simba
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (wa pili kushoto) akipiga krosi huku akizongwa na mabeki watatu wa Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Pius Buswita wa Yanga (kushoto) akiwania mpira na beki wa Simba Mohamed Hussein
Emmanuel Michael, akipiga shuti langoni mwa Simba
Ajib (kushoto) akipongezana na Hussein baada ya mchezo huo kumalizika
Ajib akipongezana na Niyonzima baada ya mchezo huo kumalizika.























No comments:
Post a Comment