BODI
YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAARIFA
KWA UMMA
UFAFANUZI
KUHUSU UPANGAJI MIKOPO KWA 2017/2018
Novemba
6, 2017
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu sifa na taratibu za utoaji
mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Taarifa hii inalenga kutoa ufafanuzi
kufuatia maoni ya baadhi ya wadau kuwa baadhi ya waombaji mikopo wenye sifa
wanakosa mikopo ya elimu ya juu.
i.
Uyatima:
Waombaji ambao wamefiwa na wazazi na hivyo kushindwa kumudu gharama za elimu ya
juu. Kwa mwaka huu, waombaji yatima wanapaswa kuthibitisha uyatima wao kwa
kuwasilisha vyeti vya vifo vya wazazi wao vilivyothibitishwa na Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);
i.
Wenye
ulemavu: Waombaji wa mikopo wenye ulemavu wanapaswa kuambatisha
barua kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa inayothibitisha ulemavu huo;
ii.
Uduni
wa kipato: Waombaji ambao wanatoka kwenye familia zenye vipato duni,
miongoni mwao wakiwamo wale wenye barua za uthibitisho kuwa waliosomeshwa
kwenye masomo yao kabla ya kujiunga na elimu ya juu;
Pamoja na sifa/vigezo
hivi, kila mwombaji ni lazima awe amepata udahili au kuthibitisha udahili
katika taasisi moja ya elimu ya juu ambayo atajiunga kwa ajili ya masomo na
asiwe na umri wa zaidi ya miaka 30.
Aidha, tunapenda
kufafanua kuhusu takwimu za utoaji mikopo kwa mwaka 2017/2018 kama ifuatavyo:
i.
Bajeti ya jumla ya mikopo kwa mwaka 2017/2018
ni TZS 427.54 bilioni kwa ajili ya
jumla ya wanafunzi 122,623. Fedha
hizi zinajumuisha malipo ya ada za wanafunzi wenye mikopo pamoja na fedha za
chakula na malazi, vitabu n.k;
ii.
Fedha zinazohitajika kwa malipo kwa ajili ya
Robo ya Kwanza ya mwaka 2017/2018 ni TZS
147.06 bilioni ambazo tayari Bodi imeshapokea kutoka Serikalini;
iii.
Hadi leo, Novemba 6, 2017, jumla ya wanafunzi 29,578 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa
mikopo yenye thamani ya TZS 96.5 bilioni na fedha zao tayari zimeshatumwa vyuoni
ili kuwawezesha kuanza masomo;
iv.
Aidha, fedha za mikopo ya wanafunzi wote
wanaoendelea na masomo zimetumwa vyuoni ili kuwawezesha kuendelea na masomo.
Kufunguliwa
kwa dirisha la rufaa
Tunapenda pia
kuwajulisha waombaji wa mikopo wote kuwa dirisha la rufaa litafunguliwa
Jumatatu, Novemba 13, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika
kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. Maelezo ya kina yatatolewa
kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).
Tunatoa wito kwa uongozi
wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya
Mikopo. Lengo ni kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa rufaa zao ifikapo
Novemba 30, 2017.
Imetolewa na:
(Signed)
Abdul-Razaq Badru
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 6, 2017

No comments:
Post a Comment