Meneja Uhusiano toka Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Jumaa Almasi (kulia) akielezea mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa Rais John Pombe Magufuli mapema hii leo Jijini Dar es Salaam, (kushoto) ni Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Mvungi.
Meneja Uhusiano toka Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Jumaa Almasi (katikati) akielezea mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa Rais John Pombe Magufuli mapema hii leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Mvungi na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Fatma Salum.
Afisa Uhusiano toka Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Patrick Mvungi (kushoto) akielezea mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa Rais John Pombe Magufuli mapema hii leo Jijini Dar es Salaam, katikati ni Meneja Uhusiano wa taasisi hiyo Jumaa Almasi na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Fatma Salum. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
**********************************
Na Fatma
Salum (MAELEZO)
Taasisi ya
Tiba ya Mifupa (MOI) imenufaika na mabadiliko chanya yaliyofanyika ndani ya
miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe
Magufuli.
Mabadiliko
hayo yameboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira bora kwa watoa
huduma jambo ambalo limeleta faraja kwa wananchi wanaofika kwenye taasisi hiyo
kupata huduma mbalimbali za tiba ya mifupa.
Hayo
yameelezwa leo na Meneja Uhusiano wa MOI Jumaa Almasi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo kwenye miaka miwili ya uongozi
wa Rais Magufuli.
“Maboresho
yaliyofanyika katika kipindi hiki kifupi yameiwezesha MOI kutoa huduma bora kwa
wakati ukilinganisha na miaka mingine iliyopita,” alisema Almasi.
Akifafanua
kuhusu maboresho hayo, Almasi alisema kuwa kwa sasa MOI kuna ongezeko la
vitanda vya kulaza wagonjwa kutoka vitanda 159 hadi 340 hivyo hakuna tena
changamoto ya wagonjwa kulala sakafuni.
Alieleza kuwa
idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji imeongezeka hadi kufikia wagonjwa 700
kwa mwezi kutokana na Serikali kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba na nafasi ya
kulaza wagonjwa.
Aidha
alisema kuwa katika kipindi cha miaka miwili kuna ongezeko la wagonjwa wanaopata
huduma za kibingwa MOI (Super Specialized Services) ambapo idadi kubwa ya
wagonjwa wameweza kufanyiwa upasuaji mkubwa wa nyonga, mgongo, ubongo, upasuaji
wa matundu, magoti, kiuno pamoja na upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na
mgongo wazi.
Kwa upande
mwingine Afisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi alieleza kuwa pamoja na upasuaji
mkubwa uliofanyika katika kipindi hiki pia viungo bandia 1,362 vimetengenezwa
kutokana na Serikali kurahisisha upatikanaji wa malighafi za kutengenezea
viungo hivyo.
“Awali
wagonjwa wengi walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa gharama kubwa ili kuwekewa
viungo vya bandia, lakini sasa wanaweza kupata huduma hiyo wakiwa hapa hapa
nchini,” alisema Mvungi.
Mvungi
alieleza kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha
mradi wa MOI awamu ya tatu (MOI Phase III) ambapo zitatumika kununulia vifaa
ikiwemo CT SCAN, MRI, mashine mbili za XRAY na Ultrasound ya kisasa.
Pia Serikali
imekuwa ikiwajengea uwezo wataalamu wa hapa nchini kwa kuleta wataalamu wengine
kutoka mataifa mbalimbali duniani ili waweze kujifunza na kubadilishana uzoefu.



No comments:
Post a Comment