Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara, wakwanza kushoto ni
mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi
wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo
Hiiti B. Sillo.
. Ummy
Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa uzinduzi wa
maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na
Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa.

Watumishi wa
umma na wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa iliyokuwa
ikiwasilishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(MB) hayupo kwenye picha,
mapema leo katika uzinduzi wa Maabara hamishika uliofanyika katika ofisi za
TFDA.
Meza
kuu ikiongozwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja wakati wa
uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula,
Dawa na Vipodozi.
*******************************************
Na WAMJWW
Wawekezaji wa ndani wanao taka
kujenga viwanda vya dawa wahimizwa kuhakikisha wanakidhi vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza
kuruhusiwa kufanya shughuli hiyo ya uzalishaji wa dawa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua maabara hamishika zakudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema
leo katika viunga vya mamlaka ya dawa, chakula na Vipodozi (TFDA)
Aidha Mh. Ummy ameahidi kuongeza
jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa
kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa mbao ulianza 2002 unaohusu uchunguzi wa Dawa
muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Maleria pamoja na Viuwa sumu.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy amesisitiza athari za uwepo wa dawa
zisizo na ubora katika jamii ikiwepo kuhathiri
uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana na kmanunuzi
ya Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa
kutibu mwisho hupelekea usugu wa Dawa katika mwili.
Waziri Ummy hakusita kuipongeza Bodi
, Uongozi na wafanyakazi wa TFDA kwa
utendaji mzuri wa kazi huku akiahidi kuendelea mkuwaunga mkono
kwa kushirikiana nao kwa ukaribu katika safari ya kumsaidia Raisi wa Jamhuri ya
Tanzania Dkt. John Magufuli.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti
Sillo alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia
kuwabaini na kuwakamata wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri
jamii na uchumi kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa dawa bandia
ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017 imeshuka kwa chini ya 1%” , alisema Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)
Hiiti Sillo, huku akisema
mafanikio hayo yanatokana na ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na taasisi hiyo.
Bw. Hiiti Siilo aliendelea kwa kusema
kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake TFDA imepanga kupeleka maabara hizo
katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo ikiwemo ofisi ya Tabora,
Hospitali ya Mbeya na Mtwara huku
nyingine zitapelekwa katika vituo vya Forodha Namanga,KIA mpakani, Silali (Tarime)
na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, alisisitiza Bw. Sillo.




No comments:
Post a Comment