Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
(wapili kulia.) akiwa katika picha ya pamoja na timu iliyoshinda fainali za
mashindano ya mabenki yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa
Uhuru aliyeshika kombe ni Kapteni wa Timu hiyo Bw.David Kikambako na (wa kwanza
kulia ) ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi zawadi ya mchezaji bora wa mashindano Bw.Jesse Nyambo kutoka Benki ya Exim (katikati) ni muundajia wa mashindano hayo Bi.Nasikiwa Beria.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi zawadi ya cheti cha Kapteni bora wa mashindano ya Mabenki Bw.David Kikambako kutoka benki ya DTB wa Exim Bank (katikati) ni muundajia wa mashindano hayo Bi.Nasikiwa Beria.
Mshambuliaji wa timu ya Benki ya Exim Abdallah Masoud (Katikati) akipambana katika mchuano wa fainali za mashindano ya Mabenki
*******************************************
************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
Waziri wa Habari
utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameto wito kwa sekta
mbalimbali nchini kutoa fursa za wafanyakazi wake kushiriki katika michezo
wawapo kazini kwani michezo ni afya.
Mheshimiwa Mwakyembe
ametoa wito huo alipokuwa akifunga fainali za mashindano ya michezo ya mabenki yaliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam katika uwanja wa Uhuru.
“Natoa pongezi kwa
taasisi zote benki zilizoshiriki katika mashindano haya kwa michezo ni afya na inaongeza
utendaji mzuri kazini pamoja na kuongeza umoja miongoni mwa
wafanyakazi,”Mhe.Dkt. Mwakyembe.
Naye Muandaaji wa mashindano
hayo Bi Nasikiwa Beria alisema kuwa anashukuru serikali kwa kuwaunga mkono na
katika mashindano hayo kwani imewapa hamasa zaidi na kwa mwakani watajitahidi
mashindano haya yafanyike pia na mikoani tofauti na mwaka huu yalivyofanyika
hapa jijini Dar es Salaam.
“Mashindano haya kwa
mwaka huu yalihusisha benki kumi na tano
na kulikuwa na michezo sitini na tulianza michuano kuanzia mwezi wa nane
na fainali ndiyo zimefanyika mwezi huu Desemba na kwa mwakani tunampango wa
kuongeza michezo iwe ya aina mbalimbali ikiwemo Volleyball na
Netiboli,”Bi.Beria.
Kwa upande wa Mkurugenzi
wa Exim Benki ambaye jina lake halikuweza kujulikana kwa haraka alitoa pongezi
na zawadi ya shilling laki moja kwa kila mchezaji wa timu ya ofisi yake kwa
kuibuka washindi wa pili katika mashindano hayo .
Pamoja na hayo na
Kapteni wa Timu ya DTB Benki Bw.David
Kikambako alishukuru viongozi wa benki zilizoshiriki kwenye mashindano hayo na
kutoa wito kwa benki nyingine kujitokeza kujiunga katika mashindano hayo kwa
mwakani .
Katika mashindano hayo
Benki ya DTB iliibuka kidedea kwa penati tatu dhidi ya Timu ya Exim Benki.
No comments:
Post a Comment