Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo (Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Naibu Waziri OR
TAMISEMI, Joeseph George Kakunda baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba
wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi
kilichofanyika mjini Dodoma
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo (Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Naibu Waziri OR
TAMISEMI, Josephat Sinkamba Kandege baada ya zoezi la kupitia na kusaini
Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao
kazi kilichofanyika mjini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimpatia Mkataba wa Huduma za Lishe Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhandisi Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo (Mb) akisani Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za
Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo, na waliosimama ni Naibu Mawaziri na Watendaji OR
TAMISEMI wakishuhudia zoezi hilo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mawaziri OR TAMISEMI
na Wakuu wa Mikoa baada ya zoezi la kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi
na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi kilichofanyika
mjini Dodoma
***********************************************
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
(Mb) amewaongoza wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, kupitia na kusaini Mkataba
wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa, kikao kazi
kilichofanyika mjini Dodoma.
Akiongea na Wakuu wa Mikoa
katika ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma, Mhe. Jafo amesema maelekezo hayo awali,
yalitolewa na Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu, kuhusu tatizo
la Lishe katika Mikoa nchini ambalo nchi imekwishajitoa kulishughulikia na
kutenga fedha katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2017/2018.
“Tumesaini hii mikataba kwa
lengo kubwa la kuhakikisha kwamba Wakuu wa Mikoa kama ndio viongozi wa Wakuu wa
Mikoa, wahakikishe halmashauri zao zinaenda kutekeleza mipango yao ya bajeti
ambayo imetengwa katika halmashauri zao kwa lengo kubwa kwamba, tunaenda
kutekeleza tatizo la lishe ndani ya halmashauri zetu”
Mhe. Jafo amesema Wakuu wa
Mikoa wanayo dhamana kubwa ya kusimamia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa
vituo vya afya na suala la lishe kwa ujumla, hivyo Watendaji watoe taarifa zao
kwa Wakuu wa Wilaya kabla ya kuwasilishwa kwa Wakuu wa Mikoa kwa hatua stahiki.
“Wakurugenzi watoe taarifa
kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Wilaya nao wawasilishe kwa Wakuu wa Mikoa ili
waone namna ya kuzisemea taarifa hizo”, katika suala zima la utekelezaji wa
mipango ya Serikali.
Aidha, amewataka Wakuu wa
Mikoa kuwaelekeza na kuwasimamia Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya
masuala ya lishe na ujenzi wa vituo vya afya kwani mpaka sasa jumla ya vituo
2011 vimepanuliwa na kujengwa ili kutoa huduma bora kwa jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
Dkt. Kebwe S. Kebwe amesema, anaipongeza Serikali kwa kutoa takribani shilingi
11.6 Bilioni kwa ajili ya suala la lishe hasa katika kipengele cha udumavu.
Aidha, amesema suala zima la
upatikanaji wa chakula mkoani Morogoro sio tatizo bali ni elimu ya ulaji
chakula ndiyo inapaswa kutolewa ili kupunguza utapiamlo lakini pia kumekuwepo
na tatizo la Maafisa Lishe katika halmashauri nchini kupangiwa kazi nyingine,
kwa mfano kufanya kazi ya Idara tofauti kama vile kukusanya kodi.
Naye Stephen Motambi, Kaimu
Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema
suala la Lishe limekuwa likifanyika katika Mikoa na Halmashauri zote katika
kukabiliana na tatizo hili lakini kwa hivi sasa hali ya udumavu ni asilimia 34
hivyo mikoa inapaswa kuweka mikakati kuhusiana na kuondoa kabisa tatizo la lishe.
No comments:
Post a Comment