Habari za Punde

SEVILLA WALIVYOMNYAMAZISHA MANARA TAIFA 5-4

Mshambuliaji wa Seville, Wissam Ben Yedder (katikati) akichuana kuwania mpira na mabeki wa Smba Erasto Nyoni (kushoto) na Pascal Wawa, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana usiku. Katika mchezo huo Sevilla ilishinda mabao 5-4.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, akimkabidhi kombe Nahodha wa Sevilla, Ever Banega, baada ya kuifunga Simba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Sevilla walishinda mabao 5-4. 
Mchezaji wa Sevilla Fc, Sergio Escudero, akipiga shuti katikati ya mabeki wa Simba na kuifungia bao la kwanza timu yake wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki akwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, jana.
Skauti wakiziba barabara kuzuia magari na watu wasiohusika kutumia geti kuu.
Mjasiriamali akisubiri wateja wa kununua skafu za simba...
Mchezaji wa Sevilla akiingia uwanjani
Waziri Mwakyembe akisalimiana na wachezaji wa Sevilla.
Wachezaji wa timu ya Sevilla wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao baada ya kukabidhiwa.
John Bocco, akijaribu kumhadaa kipa wa Sevilla, Thomas Vaclik, wakati wa mchezo huo. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la nne wakati wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla Fc ya Hispania kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Sevilla walishinda mabao 5-4. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la nne wakati wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla Fc ya Hispania kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Sevilla walishinda mabao 5-4. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.