Habari za Punde

TIMU YA TAIFA STARS YAWATIA MOYO WATOTO WA KLINIKI YA YOUTH SOCCER

 Wachezaji wa timu ya Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Ur 11

Mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars, Simon Msuva, akicheza soka na watoto umri chini ya miaka 11 wa kituo cha Karume Academy wakati timu ya Taifa ilipotembelea Kliniki ya watoto 'Youth Soccer Clinic' iliyoratibiwa na Afrisoccer kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Laureate iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Muhidin Sufiani).
 Mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars, Iddi Seleman, akicheza soka na watoto umri chini ya miaka 11 wa kituo cha Karume Academy wakati timu ya Taifa ilipotembelea Kliniki ya watoto 'Youth Soccer Clinic' iliyoratibiwa na Afrisoccer kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Laureate iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
 Watoto wakijaribu kuonyesha vipaji vyao 
******************************************
Na Dina Mgana
TIMU ya Taifa  ya Tanzania Taifa Stars inayotarajia kushuka dimbani keshokutwa katika mchezo wa kufuzu Afcon 2021, leo imetembelea Kliniki ya watoto wachezaji  iliyoandaliwa na  AfriSoccer kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya ‘Laureate International’  iliyopo Mbezi Beach Jijini Dar es salaam.
Katika ziara hiyo wachezaji hao walipata fursa ya kuzungumza na watoto hao na kucheza pamoja huku wakiwaasa kupenda michezo na kuzingatia masomo ili waweze kufikia malengo yao yao ya kimichezo.
Akizungumza katika ziara hiyo Nahodha wa timu yatifa, Mbwana Samatta, aliwapongeza waandaaji wa Kliniki hiyo kwa kuweza kuwakusanya watoto na kuwapa elimu ya Soka na kuwakutanisha na wachezji wa timu ya Taifa ili kuwapa hamasa.
‘’Hata sisi pia tulikuwa kama ninyi na tulikuwa na ndoto za kufika hapa tulipo kwa sasa lakini njia pekee ni kufuata maelekezo ya walimu wenu wa michezo na shuleni, kuzingatia ratiba ya mazoezi na kutojihusisha na makundi yasiyofaa’’. Amesema Samatta.

Kliniki hiyo imehusisha watoto wa Kituo cha TFF na Shule ya Sekondari ya Laureate ambapo waliweza kucheza mechi pamoja na michezo mingine.
 Mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars, Simon Msuva, akicheza soka na watoto umri chini ya miaka 11 wa kituo cha Karume Academy wakati timu ya Taifa ilipotembelea Kliniki ya watoto 'Youth Soccer Clinic' iliyoratibiwa na Afrisoccer kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Laureate iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, leo.
 Nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto.

 Kipa wa timu ya Taifa, Juma Kaseja akiwafundisha makipa watoto
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.