Habari za Punde

TRENI YA KRISMASI YAONDOKA DAR LEO WAZIRI ISAACK KUPANGA FOLENI YA KUKATA TIKETI

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe, akizungumza na abiria aliyesafiri na Treni ya Reli ya kati leo jioni kuelekea Kaskazini Mkoani Moshi wakati alipofika kuwaaga na kuzungumza na abiri hao waliosafiri kuelekea katika Sikukuu ya Krismasi mkoani humo.  (Picha na Muhidin Sufiani)
****************************************
Akizungumza na waandishi baada ya kuwaaga abiria hao Waziri Kamwelwe, alisema kuwa kutokana na ongezeko la abiria, tayari Serikali imeagiza mabehewa 45 mapya kwa ajili ya kutatua changamoro ya msongamano wa abiria wanaotumia Reli ya kati.
Aidha alisema kuwa mpaka sasa tayari jumla ya abiria 6,500 wamekwisha safiri na Treni hiyo tangu ilipozinduliwa safari hiyo ya Reli ya kati na kwamba bado idadi hiyo inaongezeka na hasa kuelekea kipindi cha sikukuu za mwisho mwaka.
Ratiba ya Treni hiyo imeongezeka siku moja na kuwa mara tatu kwa wiki badala ya mara mbili kwa wiki kutokana na ongezeko la abiria ambapo Treni hiyo leo imeondoka na jumla ya abiria 950.
''Ratiba ya usafiri itabadilika na kuongezeka siku moja ya jumatatu katika kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka kwa sababu abiria wanaotumia usafiri huu wameongezeka'' alisema Kamwelwe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti abiria waliosafiri na Treni hiyo walisema kuwa katika Usafiri huo changamoto kubwa ni msongamano  wa abiria ambao huchukua muda mrefu kupata tiketi kutokana na wingi wa abiria na vituo kuwa vichache ambapo Waziri Kamwelwe, alisema kuwa siku ya jumatatu atafika eneo hilo kukata tiketi yeye mwenyewe ili kujionea changamoto hilo ziweze kufanyika kazi kwa haraka. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe, akipeperusha bendera kuashiria kuwaaga abiria waliosafiri na Treni ya Moshi kutoka jijini Dar es Salaam, leo jioni kuelekea Kaskazini katika Sikukuu ya Krismasi. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa na Ofisa Habari wa Shirika hilo, Jamila Mbarouk.
 Waziri Kamwelwe na baadhi ya viongozi wakipunga mikono kuwaaga abiria
 Waziri Kamwelwem akizungumza na abiria ndani ya behewa kabla ya kuanza safari.
Waziri Kamwelwe akishuka katika Treni hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.