Habari za Punde

TRC, POLISI WAZINDUA KAMPENI, WATOA ONYO KWA WEZI NA WAHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA RELI

 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usalama wa Reli kwa kuzuia ajali, uhalifu na hujuma katika Reli ya Shirika hilo, ambayo itakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa Rasilimali za shirika hilo. Katikati ni Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi Stanslaus Kulyamo (kushoto) ni Ofisa Habari wa Shirika hilo, Jamilla Mbarouk. (Picha na Muhidin Sufiani).
 Ofisa Habari Jamilla Mbarouk, akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo na waandishi wa habari.
 Na AMINA KASHEBA
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limetoa onyo kali dhidi ya watu wanaolenga kufanya wizi dhidi ya miundombinu ya reli, na kutaka kila mtanzania kuwa mlinzi wa rasilimali hiyo ili kukuza uchumi na kurahisisha usafiri nchini.
Aidha shirika hilo limewataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kutambua thamani ya miundombinu mbalimbali ikiwamo reli katika ustawi wa jamii ili kuepuka kufanya hujuma mbalimbali.
Onyo hilo linakuja ukiwa ni mwezi mmoja umepita tangu watu wasiojulikana walipong’oa vyuma vya reli katika eneo la Kahe, Kisangilo mkoani Kilimanjaro  na kusababisha usafiri wa treni ya Dar es Salaam -  Moshi kushindwa kuendelea na utoaji huduma kwa wananchi Kisangilo hadi kuleta changamoto hiyo ilipotatuliwa na mafundi wa TRC.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji  TRC, Focus Makoye alisema  baaada ya kutokea kwa uharibifu wa miundombinu ya njia ya reli na wizi wa vyuma  leo wamezindua kampeni  hiyo ya usalama na utoaji elimu  kwa wananchi kujua umuhimu wa reli.
"Kampeni hii ni mathubuti kwa watanzania kufahamu umuhimu wa reli kwa ajili ya kuepusha matatizo mbalimbali kama wizi wa vyuma vya reli uharibifu wa miundombinu na ufanyaji kazi kando ya reli," alisema.
Alisema  kwa ushirikiano na Shirika la Reli Tanzania TRC  na jeshi la polisi kwa pamoja wasimamia zoezi hilo na kutoa elimu kwa wananchi kwa ajili ya kuondoa matatizo yanayotokea katika reli ambayo yanaleta athari na kusababisha ugumu wa usafiri  kwa watanzania.
''kabla ya kuchukua maamuzi ya kuzindua kampeni hiyo watu wasiojulikana walikuwa wakiweka mawe makubwa katikati ya Reli kwa lengo la kuiangusha Treni, lakini kwa umakini wa wafanyakazi wa Shirika letu waliweza kugundua na kufanikiwa kuyaondoa mawe hayo makubwa kabla ya Treni kupita'' alisema Sahani
Kwa upande wa msaidizi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Reli, Stanslaus Kulyamo, 
 alisema wamejipanga vizuri katika maeneo yote kwa ajili kusimamia ulinzi kwa kulinda miundombinu ya reli ili watanzania waweze kupata usafiri kwa haraka.
Aliongeza kuwa kila mtanzania anatakiwa kuwa mlinzi wamwenzake ili kulinda uhalibifu wa miundombinu ya watanzania wote inayotumia ghalama kubwa kuijenga, na kuongeza kuwa kwa yeyote atakayekamatwa akifanya hujuma ya miundombinu ya taifa atakuwa ni mfano kwa watanzania wote.
“Hii ni kampeni kabambe ambayo kila mtanzania anapaswa kufahamu umuhimu na sheria zilizopo katika reli kwa ajili ya kuepukaa wizi na uharibifu wa miundombinu inayotokeaa katika njia ya treni,”alisema.

Kwa upande wa wananchi, Sarah Joseph Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, alisema kuwa 
kampeni ni muhumu kwa watanzania ambao wengi hawajui umuhimu na faida ya kulinda Raslimali za Taifa na wengine waliozoea kufanya kazi karibu na njia ya Treni.
“Watanzania tunatakiwa kulinda rasimali zetu ambazo ndio msingi kubwa wa maendeleo nchini tunapoaharibu miundombinu ni jambo la kutia aibu kwa serikali, “alisema.
 Upande wa Michael Mussa alisema serikali inatakiwa kuwachukulia hatua kali wale wanaoharibu miundombinu ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Tukio hilo lilitokea Disemba 25  mwaka  jana katika eneo la Kahe, Kisangilo Mkoani Kilimanjaro,  watu wasiojulika kwa kung’oa mataruma ya Reli na  vifaa vya kuunga reli na reli  watu hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuchukuliwa hatua.
Kamanda akizungumza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.