Habari za Punde

MKUTANO WA KUWANADI WAGOMBEA JIMBO LA MWERA WAFUNIKA, MWNACHAMA WA CUF ARUDISHA KADI


MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Kessy Ramadhan Mussa (kulia) akimtambulisha mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwera, Zahor Mohammed Haji, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani, mjini Unguja, jana. MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mwera, Zahor Mohammed Haji, akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani mjini Unguja jana. Katika mkutano huo aliyekuwa mwanachama wa CUF, Adam Hassan Mohammed, alirudisha kadi ya CUF na kujiunga na CCM. Sehemu ya wananchi na wanachama wa CCM wakishangilia wakati akitambulishwa mgombea Ubunge wa Jimbo lao la Mwera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani jana.Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mfenesini, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Mwera, alipowatambulisha wagombea wa jimbo hilo jana.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwera, Zahor Mohammed Haji, akimtunza msanii wa mashahiri, wakati wa mkutano huo.
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Kessy Ramadhan Mussa, akimtambulisha mwanachama mpya, aliyerudisha kadi ya CUF na kujiunga na CCM akitokea chama cha CUF, Adam Hassan Mohammed, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani mjini unguja jana. 
Wasanii wa Beni Bati wakitoa burudani
Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Mwera, Mihayo J. N'hunga, akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani mjini Unguja jana. Katika mkutano huo aliyekuwa mwanachama wa CUF, Adam Hassan Mohammed, alirudisha kadi ya CUF na kujiunga na CCM. 
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Kessy Ramadhan Mussa (kulia) akimtambulisha mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mwera, Mihayo J. N'hunga, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mwera Mahakamani, mjini Unguja, jana. 
Wasanii wa maigizo wakitoa burudani
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitoa burudani
Viongozi wakiagana baada ya mkutano hu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.