Habari za Punde

WABUNGE WAMPONGEZA KASSIM MAJALIWA KUPITISHWA JINA LAKE KUCHAGULIWA KUWA WAZIRI MKUU

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Job Ndugai, akionesha jina la Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, lililofikishwa Ukumbi wa Bunge na Mpambe wa Rais ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na kupigiwa kura ili uwa Waziri Mkuu, wakati wa Kikao tatu Bunge la 12 kilichofanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo. Katika Kikao hicho Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa amepata jumla ya kura 350 sawa na asilimia 100 na hivyo kuwa Waziri Mkuu kwa awamu ya pili baada ya kuchaguliwa na wabunge wote waliohudhuria kikao hicho. (Picha na Muhidin Sufiani)
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Mbunge wa Jimbo lwa Ruagwa, Majaliwa Kassim Majaliwa, baada ya jina lake kuteuliwa kupigiwa kura ya kuchaguliwa na Wabunge kuwa Waziri Mkuu, wakati wa kikao cha tatu Bunge la 12 kilichofanyika katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mpambe wa Rais akiwasili Ukumbini akiwa na Bahasha yenye jina la Waziri Mkuu aliyependekezwa na Rais kupigiwa kura na wabunge.
Baadhi ya Wabunge wakiwa katika kikao hicho leo, kutoka (kulia) ni Makame Mbarawa, Zahor Mohammed Haji, Turki, January Makamba na Sylivestry Koka.
Sehemu ya Wabunge ndani ya Kikao hicho
Katika Kikao hicho, pia aliapishwa Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.