Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Karakana kubwa ya kisasa ya kutengeneza Vichwa vya Treni za Umeme, kutoka kwa Mkurugrnzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC, Masanja Kadogosa, inayojengewa eneo la Kwala wakati alipofika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kukagua maendeleo ya Ujenzi huo jana. (Picha na Muhidin Sufiani)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na baadhi ya viongozi wa shirika hilo, wakati alipofika kukagua mae ndeleo ya mradi wa ujenzi wa Karakana kubwa ya kisasa ya kutengeneza mabehewa na vichwa vya Treni za umeme inayojengwa katika eneo la Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, jana.

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akizungumza na wafanyakazi wana Viongozi mbalimbali wa Shierika la Reli Tanzania TRC, wakati alipofika eneo la Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana za kuengenezea Mabehewa na Vichwa vya Treni za umeme.
********************************
Na MUHIDIN SUFIANI, PWANI
IKIWA ni siku chache tu baada ya kuapishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu kwa awamu ya pili, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,leo ameanza kazi kwa kutembelea miradi mikubwa ya Serikali na kutoa maagizo kwa watendaji.
Katika ziara yake Waziri Mkuu alitembelea mradi wa Mawalimu Nyerere wa Mabwawa ya kufua umeme unaoendelea kutekelezwa eneo la Mto Rufiji mkoa wa Pwani.
Baada ya kutembelea mradi huo Waziri Mkuu aliwasili eneo la Kwala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha nakutembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Karakana za kutengeneza Mabehewa na Vichwa vya Treni.
Akiwa Kwala Waziri Mkuu ametembelea na kukagua miradi mikubwa ya kimaendeleo ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha ahadi zote zilizohaidiwa kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inakamilika kwa wakati.
Akiwa katika mradi wa stesheni kubwa ya Karakana ya kutengeneza mabehewa na vichwa vya treni uliopo Kwala Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani, Majaliwa alisema kuwa mradi huo wa reli wa kimataifa unararajia kukamilika kwa awami ya kwanza mnamo mwezi Aprili mwakani.
Aodha akisema kuwa mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na janga la Cotona lililoikumba dunia kwa ujumla ambapo baadhi ya vifaa vilishindwa kufika nchini kwa wakati.
''Mradi huu utakapokamilika wananchi watafurahia rasilimali za taifa,
Nilipokuwa natoka Dodoma nilisimama Morogoro kituo cha kati kuona ujenzi wa phase one, nimeambiwa mwezi wa tatu au wa nne hivi maajabu yataanza safari za Dar Morogoro zitakuwa fupi zaidi, aidha mwezi Desemba mwaka huu watakamilisha kupanga mataluma kwa kilomita 50 hadi 60 zilizobaki ili viberenge vianze kupita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na nitakuwa wa kwanza kupanda." alisema Majaliwa.
Alisema kuwa ni mara ya tano anatembelea mradi huo kwa nyakati tofauti na kujionea maendeleo makubwa na ahadi zote zilizohaidiwa zitatekelezwa kwa wakati.
"Nimeridhika na utendaji na usimamizi wa kazi, fedha zinazotekeleza mradi huu na hata ule wa umeme wa Mwalimu Nyerere ni kodi za Watanzania wenyewe ambao miongoni mwao wamefaidika na miradi hii kwa kuajiriwa na niwahakikishie na kuwataka watanzania kuendelea kuiamini Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli kwa nguvu waliyoionesha siku chache tu zilizopita Oktoba 28 katika uchaguzi."
Ameeleza kuwa Shirika la Reli nchini (TRC,) limekua likifanya kazi kwa weledi kama lilivyoaminiwa na Serikali.
"TRC safi sana, mnafanya kazi nzuri na mradi huu unaotekelezwa na kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini Uturuki umeendelea kudumisha mahusiano mema."alisema.
Akiwa eneo hilo la Kwala Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Butamo Ndalahwa, kuhalakisha mchakato wa maombi ya hekari 4000 zilizoombwa ili wawekezaji waanze kujenga miundombinu ya kiuchumi ikiwamo hoteli na sehemu za biashara kwa kuwa sehemu hiyo ni kituo kikubwa cha reli hiyo ya kisasa kitakachokuwa na zaidi ya wafanyakazi 500.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kagogosa alisema kuwa wataendelea kutekeleza miradi muhimu ya kimaendeleo ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi jirani katika kuhakikisha maendeleo yanawafikiwa zaidi wananchi. Aidha Kadogosa alisema miradi yote inayosimamiwa na Shirika hilo itatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kufaidi matunda ambyo Serikali ya awamu ya tano imekua ikiitekeleza usiku na mchana.
Waziri Mkuu akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Butamo Ndilahwa, akimsisitiza kufanya haraka mchakato wa kufuatilia kuta Hekari 4000 kwa ajili ya wawekezaji na wananchi watakaohitaji kuwekeza katika enep hilo.
Mnara wa Mawasiliano unaojengwa eneo hilo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na baadhi ya viongozi wa shirika hilo, wakati alipofika kukagua mae ndeleo ya mradi wa ujenzi wa Karakana kubwa ya kisasa ya kutengeneza mabehewa na vichwa vya Treni za umeme inayojengwa katika eneo la Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, jana.
Jengo la Utawala

Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Yapi Merkez baada ya kukagua mradi huo.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika hilo la TRC baada ya kukagua mradi huo.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Yapi Merkez baada ya kukagua mradi huo.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hilo baada ya kukagua mradi huo.
Muonekano wa ujezi wa Reli hiyo ikiwa tayari imewekwa milingoti ya Umeme
Jengo la Utawala
No comments:
Post a Comment