Habari za Punde

WILAC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA KUPINGA UNYANYASAJI WA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAFUNZI

Mratibu wa mradi wa Ulinzi kwa watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kutoka Kituo cha msaada wa Sheria Tanzania (WILAC,) Abia Richard akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tandika, wakati ujumbe kutoa WLAC ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi ikiwa ni muendelezo wa kuzidi kuwajengea uwezo na kuwawezesha kujiamini kuhusu Unyanyasaji wa Kijinsia.
Abia amewataka watoto hao kutosita kupindi waonapo matukio ya unyanysaji.
Abia akiserebuka na wanafunzi wa Shule ya msingi Temeke wakati alikuwa akiwasili dhuleni hapo na kupokelewa kwa nyimbo.

KITUO cha msaada wa Sheria kwa Wanawake Tanzania (WILAC,) kimeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi kuhusiana na vitendo vya unyanyasaji na namna ya kukabiliana navyo.
Kupitia mradi wa Ulinzi kwa mtoto unaotekelezwa na WILAC kwa Shule kumi za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam watoto wengi wamepata msaada dhidi ya vitendo vya ukatili walivyofanyiwa pamoja na elimu ya kuepukana na kuripoti matukio hayo.
Leo Februari 17, Timu ya WILAC imetembelea shule za Msingi za Tandika na Temeke na kutoa elimu kwa njia ya sanaa ili kuwalinda watoto.
Shule zinazonufaika na mradi huo ni pamoja na Shule za msingi Tandika, Temeke, Mbagala, Kingugi, Mbaagala Annex, Mzimuni Magomeni, Kawe A, Mburahati, Tandale Magharibi na Hananasif.
Wakipozi katika picha
Baadhi ya wanafunzi wakivaa beji zeny ujumbe wa kupinga unyanyasaji baada ya kugaiwa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.