Habari za Punde

WLAC YAWAKUTANISHA WALIMU, MAPOLISI, MADAKTARI, MAHAKIMU, WANASHERIA NA USTAWI WA JAMII KUJADILI CHANGAMOTO KATIKA ULINZI NA KESI ZA UBAKAJI NA ULAWITI WA WATOTO

Wakili wa Kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake WLAC na Meneja wa Idara ya Ufuatiliaji na tathmini Wigayi Kisandu,   akizungumza wakati akifungua rasmi mkutano wa wadau wa WLAC, Walimu, Madaktari, Mahakimu Mapolisi, Wanasheria na Ustawi wa Jamii, waliokutanishwa kwa pamoja na kituo hicho kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika ulinzi  na kesi za ubakaji na ulawiti.

Akizungumza katika mkutano huo Kissandu, alisema kuwa WLAC imegundua kuwa changamoto zimekuwa nyingi na huku kila mmoja akimtupia mpira mwenzake kuwa huenda ndiye anasababisha kuchelewa kwa kesi za watoto na ndiyo sababu kubwa iliyofanya kuwakusanya wadau wote hao kwa pamoja ili kujadili kwa kina na kupata suluhishi.

Kutokana na mvutano mkubwa uliobuka katika mkutano huo huku kila mmoja akimtupia mpira mwenzake wadau wameomba kuandalia kipindi maalumu cha malumbano ya hoja kupitia Televisheni ya ITV ili wasikilizaji pia waweze kuchangia kwa kina na kupata suluhisho.

Aidha Kisandu alisema kuwa lengo kubwa la kuwakutanisha wadau hao ni muendelezo wa semina wanazofanya kuhusu ulinzi wa mtoto, wakiamini kuwa ulinzi wa mtoto ni njia pekee ya kuona jamii inajenga msingi mzuri katika ulinzi wa mtoto.

''Sisi WLAC tunaamini kuwa ulinzi wa mtoto si jukumu la mtu mmoja lazima wadau mbalimbali waungane kwa pamoja ili waweze kujadiliana na kufanyia kazi changamoto zinazo wakabili na kuangalia wajibu wa kila mmoja ili waweze kuboresha huduma wanazozitoa ili ziweze kuleta tija katika ulinzi wa mtoto'' alisema KIsanduMajadiliano yakiendelea, Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbagala Kizuiani, Hassan Jeje, akichangia mada wakati wa mkutano huo.Mkutano ukiendelea.....................Majadiliano yakiendelea..........................Majadiliano yakiendelea.............................Mshiriki akichangia mada wakati wa mkutano huo uliokuwa na mvutano mkubwa kiasi cha kuomba kipindi cha malumbano ya Hoja katika kituo cha Televisheni cha ITV.Mratibu wa mradi wa Ulinzi kwa watoto dhidi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia  kutoka Kituo cha msaada wa Sheria  (WILAC,) Abia Richard, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Afisa mratibu mwandamizi wa Polisi kutoka Dawati Kanda maalumu Dar es Salaam, Leah Mbunda (kulia) akifuatilia majadiliano hayo.........

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.