Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS DKT, MPANGO AZINDUA KAMUSI KUU YA KISWAHILI TOLEO LA TATU JIJINI ARUSHA,

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Phillip Mpango, (wa tatu kulia) akiashiria kuzindua rasmi Kamusi Kuu ya tatu ya Kiswahili, wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani, lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Wa nne (kushoto) ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (kushoto) ni Naibu wake, Pauline Gekul, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela na Balosi za Kiswahili nchini Mama Salma Kikwete (wa pili kulia). wengine ni baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Longhon wachapishaji wa Kamusi hiyo Kuu toleo la tatu. (Picha na Muhidin Sufiani)
Makamu wa Rais Dkt, Phillip Mpango, akizungumza baada ya kuzindua rasmi Kamusi Kuu ya tatu ya Kiswahili, wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani, lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi wa China Media Group, yenye Makao Makuu yake nchini Kenya, Du Shunfong, akiwasilisha mada yake mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais,
Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa, akizungumza wakati wa Kongamano hilo,
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Inocent Shio, akiwasilisha hotuba yake wakati wa Konamano hilo.
Balozi wa Kiswahili Nchini Tanzania, Mama Salma Kikwete, akizungumza wakati wa hafla hiyo,
Burudani....
Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango, akiwatunukia zawadi ya fedha wasanii wa kikundi ya Ngoma kutoka Chuo Kikuu cha Makumila cha jijini Arusha, wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
Makamu wa Rais akiaga baada ya hafla hiyo ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.