Habari za Punde

RAIS SAMIA KUNUNUA MAGOLI YA YANGA, SIMBA SHILINGI MILIONI 5 KWA KILA BAO LITAKALOFUNGWA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa ahadi ya kununua kila bao shilingi milioni tano kwa  tii hii katika michezo yake ya Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa salamu za Rais kwa wahariri wa Vyombo vya habari walioshiriki katika Semina maalumu iliyoandaliwa na Shirika la Reli Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Aidha Msigwa alisema kuwa Rais Samia ameamua kutoa ofa hiyo ya kununua kila bao kwa timu hizo ili kuzihamasisha timu hizo kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya kimataifa baada ya kufanya vibaya katika michezo ya o ya awali iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Rais Samia kuonyesha kuwa anaizingatia michezo na kuumia pindi timu za nyumbani zinapofanya vibaya katika michuano ya Kimataifa, amesema atanunua shilingi milioni tano kwa kila bao moja litakalofungwa na Simba katika mchezo wake dhidi ya Raja Casablanca ya nchini Moroco  ukiwa ni mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa kwa simba utakao chezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi wiki hii,
Hivyo hivuo kwa Yanga itakayocheza mchezo wake wa pili wa Ligi ya Shirikisho dhidi ya T-P Mazembe kutoka Kongo mchezo utakaochezwa Jumapili wiki hii baada ya timu zote kupoteza michezo ya awali ya ugenini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.