Habari za Punde

TRY AGAIN AWATAKA MASHABIKI SIMBA KUUNGANA ILI KUWACHAPA HOLOYA KWA MKAPA

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema licha ya kuwepo kwa mapungufu ya kikosi, mashabiki watakiwa kuungana na kusapoti timu yao kuelekea katika vita vya kusaka pointi tatu zitakazowapa nafasi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC.
ba inakibarua kigumu nyumbani kwake na kuhakikisha wanahitaji kupata ushindi wa aina yoyote ili kuvuna alama tatu katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 1:00 Usiku.
Akizungumza na gazeti hili jana, Try Again alisema kulingana na kibarua kigumu cha mechi iliyopo mbele yao dhidi ya Horoya AC, jukumu kubwa liliopo kwa sasa viongozi na wachezaji kuwa wamoja ili kuongeza nguvu kushinda dhidi ya Horoya AC.
Alisema viongozi wamefanikiwa kuondoa makundi yaliyopo na sasa wanachama na wanasimba wote kuwa wamoja na kurejesha ile kauli mbiu yao ya Simba nguvu moja.
“Wanachama kushikamana kufanikisha malengo yaliyopo mbele yao ya kucheza robo fainali, suala la maboresho ya kikosi ni hapo baadae, kwa sasa wanasimba wote tunatakiwa kuwasapoti hawa wachezaji waliyoifikisha Simba katika nafasi ya kumi katika viwango vya Shirikisho la Soka Afrika katika ngazi ya klabu.
Hao ndio wameifanya Simba kuwepo hapo licha ya kuwepo na ingizo jipya akiwemo Mosses Phiri, Jean Baleke ambaye katika michezo michache waliocheza amefunga bao 4 katika ligi bado tunahitaji kuwapa muda nyota wetu wapya,” alisema Try Again.
Alisema Simba imepata vigezo vya kucheza kombe la Super Ligi kupitia wachezaji hao waliopo sasa licha ya kuamini kikosi chao kina madhaifu na kutakiwa kuboresha.
Mwenyekiti huyo alisem malengo yao ni kufanikisha kucheza michuano hiyo ya Kombe la Super ligi kwa kufanya vizuri ili Simba is hike nafasi ya tano kwenye viwango vya CAF.
“Malengo yetu tukimaliza Super ligi, tutakuwa Top five , ninaimani kufika huko tutakqpokuwa makini, viongozi tuko makini tunafanya kazi bila ya kulala wala kuchoka,” alisema na aliongeza;
Sisi ni viongozi na sio wapenzi,tunatakiwa kufanya majukumu yetu kiuweledi mkubwa, kuhusu usajili na mapugufu ya kikosi tunayaona na kufanyia kazi,” alisema Try Again.
Alisema baada ya kupata uongozi mpya wa Simba wanaendelea kufanya uteuzi wa baadhi ya wajumbe na kuwapa elimu kwa ufupi na kuanza kukutan kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya klabu ya Simba.
Try Again alisema katika kikao hicho kutajadiliwa mambo mbalimbali ikiwemo ushiriki wa timu wa Ligi Kuu, Mabingwa Afrika, Super Ligi ikiwemo ushiriki wao na wapi kufanyia maboresho.
Katika maboresho inaingia suala la usajili kama nilivyosema awali tunahitaji maboresho ya kikosi kuongeza nguvu ndani ya kikosi chetu, ujezi wa kituo cha soka kwa vijana pamoja na kufanyia marekebisho katiba yetu ili kuongeza idadi ya wanachama,” alisema Mwenyekiti wa Bodi.
Alisema Simba inahitaji kuongeza wanachama ni aina gani ni hapo bosi itakapokutana kuunda timu maalum kwa ajili ya mchakato huo, kwa sasa nguvu zao ni kuona Simba inafaniwa kushinda mechi ya jumamosi dhidi ya Horoya AC.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.