Habari za Punde

*ARGENTINA NAYO YAANZA VYEMA YAICHAPA NIGERIA 1-0

"Niacheni nishangilie bwana"Wachezaji wa timu ya Argentina, mfungaji wa bao la kwanza na la ushindi, Gabriel Heinze (mbele), Lionel Messi (kushoto) na Jonas Gutierrez, wakishangilia na kumpongezwa mwenzao, Heinze baada ya kupitati timu yake bao katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza, bao lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo uliokuwa ukichezwa kwenye Uwanja wa Ellis Park, nchini Afrika ya Kusini na kufanya timu hiyo kuwa pointi sawa na Korea katika kundi B, huku zikitofautiana kwa magoli ya kufuna, ambapo korea ana magoli 2 na Argentina goli 1.
Kocha wa timu ya Argentina Diego Maradona, akishangilia goli lililofungwa na Heinze kipindi cha kwanza. Katika mchezo huo kocha huyo alionekana kipindi chote cha mchezo kutokaa chini huku akigeuka muokota mipira kila mpira ulipokuwa wa kuruhwa kuelekea timu pinzani kitendo kilichomfanya Kamisaa wa mchezo huo kumfuata na kumuonya.

Messi akimtoka beki wa Nigeria wakati wa mchezo huo. hata hivyo leo bahati haikuwa na yake machachari huyo kutokana na kukosa magoli mengi ambayo yalikuwa yakiokolewa na kipa wa Nigeria ambaye leo alionekana kuwa ndiye 'Man Of The Mach' kutokana na jitihada zake za kuokoa michomo mingi iliyoonekana dhahiri kuwa huenda ingemshinda kipa huyo.

Diego akifoka kuwaelekeza wachezaji wake....




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.