Mchezo kati ya Korea na Greece, umemalizika hivi punde huko Afrika ya Kusini ambapo Korea wameweza kuibua wababe wa mchezo huo kwa kuwafunga mabao 2-0.
Goli la kwanza la kuwainua mashabiki wa Korea limepatika katika dakika ya 6 ya mchezo likifungwa na Lee Jueng Soo na goli la pili na la ushindi huo likifungwa na mchezaji mahiri wa Manchester United, Jisung Park, katika dakika ya 51.
Washambuliaji wa Greece watajilaumu kwa kuweza kupata nafazi kadhaa za wazi lakini umaliziaji wao ukiwa hafifu na kuwafanya kumaliza mchezo huo wakiwa hoi kwa kichapo cha mabao 2.
Mchezo unaofuata ni kati ya Nigeria na Algentina, unaotarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa huku mashabiki wa soka wakisubiri kipute cha nguvu na cha kusisimua hapo saa 3: 30 usiku kwa saa za hapa home, kati ya England na Marekani.
No comments:
Post a Comment