Habari za Punde

*CHAMPION YAZINDUA KAMPENI YA KAMPENI YA KUTANGAZA NA VYOMBO VYA HABARI

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika EngenderHealth, Dk. Dustan Bishanga, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kutumia Vyombo vya Habari, kufikisha ujumbe wa ‘Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio Tulia na Wako’, wakati huu wa michuano ya Kombe la Dunia.


Sufianimafoto, akipokea zawadi ya Tshirt yenye ujumbe wa Kampeni hiyo, wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika leo.
Wafanyakazi wa Shirika la EngenderHealth, , wakipuliza Vuvuzela, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kutumia Vyombo vya Habari wakati huu wa Mashindano ya Kombe la Dunia, ikiwa ni sehemu ya Mradi wa CHAMPION unaosimamiwa na shirika hilo wenye lengo la kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Wafanyakazi hao wakiandaa zawadi za Tisheti maalu kwa ajili ya Waandishi waliohudhulia uzinduzi huo, ili kuweza kufikisha vyema ujumbe huo kwa Jamii.

Ebwana eeh! unajua kupuliza Vuvuzela si mschezo, madada hawa wakivimba mashavu kwa ajili ya kujitahidi kupuliza hayo mananiliu......

Dk. Dustan (kulia) akimkabidhi Tisheti, mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kambi Mbwana, wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Hawa ni baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika chumba cha mkutano wa uzinduzi huo.
"VUNJA UKIMYA SEMA NA WAKO"
Ndivyo wanavyoonekana kusemezana wafanyakazi hawa wakati wakiwa kwenye uzinduzi huo...

Baada ya uzinduzi huo ilikuwa ni furaha tuuuuuuuu kwenda mbele, kwani kila mmoja alijitahidi kutaka kujua jinsi ya kupuliza Vuvuzela.....

Prepetua, akijaribu kwa nguvu zote kupuliza Vuvuzela.....bila mafanikio kwani aliishia kujaza mate tuuu kwenye dude hilo...

Eti wakishindana wakati wote hawajui kupuliza....

Dk. Dustan, akipiga mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo wa Kampeni ya Kutumia Vyombo vya Habari katika kutangaza ili kufikisha ujumbe wa Mradi wa CHAMPION.













No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.