Askari wa Kikosi cha zima moto 'FIRE', wakijadiliana jinsi ya kuwakamata madereva wote wasiokuwa na vifaa vya kuzimia moto kwenye magari yao, ambapo leo wameweza kuweka kambi ya zoezi hilo katika barabara ya Chang'ombe eneo Chuo cha VETA, jijini Dar es Salaam ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo lilianza siku za nyuma katika mtaa wa Ilala Malapa.
*VIVAZI VINGINE HIVI JAMANI HATA KAMA NI WAZUNGU HII NO....
Raia wa kigeni wakikatiza katika mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam leo mchana, huku mmoja wao akiwaacha watu hoi kwa kivazi alichokuwa ametinga, ambacho dhahili kwa maadili ya Kitanzania ni lazima kumshangaze kila aliyepata bahati ya kupishana naye mchana kweupeee, Ebwana eeh! utazani mdada huyu alikuwa eneo la sebuleni kwake ama akijiandaa kwera Room kuzifumba mboni za macho yake....Duh! Kinadada wa Kibongo mabingwa wa kuiga lakini hiii no haijatulia bwana msije kuwa kichekesho.....
*WAVUVI HARAMA KESI YAO BADO IPO IPO MAHAKA KUU DAR
*WAVUVI HARAMA KESI YAO BADO IPO IPO MAHAKA KUU DAR
Watuhumiwa wa kesi ya kuvua samaki kwenye Ukanda wa Bahari ya Hindi upande wa Tanzania, kinyume cha sheria, wakiwa kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo wakati walipofika kusikiliza kesi yao inayoendelea kwenye Mahakama hiyo.
*EBWANA EE USAFIRI MWINGINE WA HATARI JAMANI
Abiria akiwa na mzigo wa Kompyuta kwenye pikipiki, ambapo mzigo huo ulionekana kumuelemea huku akikosa mahala pa kujishikiza wakati pikipiki hiyo ikiwa kwenye mwendo eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana, bila kujali usalama wake kwanza na sijui iwapo vifaa hivyo vitaanguka anaweza kutumia gharama gani kuvitengeneza si zaidi ya gharama ambayo angechukulia usafiri wa usalama na kufika kwa usalama mahala anapokwenda????.
Eti jamaa akijificha kuogopa kamera baada ya kuona akitunguliwa mfululizo, kumbe zamaaaani tayari.
*KAHAWA KWA KASHATA KIJIWENI POOOOUWA
*KAHAWA KWA KASHATA KIJIWENI POOOOUWA
Hiki si kijiwe cha Kahawa kwa Msisiri, bali ni mahala tu walipopateuwa baadhi ya waandishi kupumzika nyakati za mchana baada ya kumaliza kazi ili kusubiri usafiri ama kazi nyingine zinazoweza kujitokeza, lakini si kupumzika pekee bali hata kujiburudisha na Gahwa kidogo, Icecream ili kuvuta mua, kama unavyowaona madada hawa Amina (kulia) akijisevia kahawa kwa Kashata si kwamba ndo msosi no, hii ni testa tu jamani.....
No comments:
Post a Comment