Hili ndilo Bango la matangazo linaloonekana katika geti kuu la kuingilia katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kwenye maonyesho ya Sabasaba..
Mafundi wakiwa katika shughuli za ujenzi na ukarabati wa sehemu za viwanja hivyo ili kuweka sawa kabla ya kuanza maonyesho hayo yanayotarajia kuanza Julai mosi mwaka huu.
Wafanyakazi wa kukodishwa katika ujenzi na ukarabati wa mabanda ya Maonyesho ya Saba Saba, wakiendelea na ujenzi ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonyesho hayo yanayotarajia kuanzanza Julai 1 mwaka huu.
Haya ni mabanda yaliyotumiwa na Wizara ya Afya katika maonyesho ya mwaka jana, ambayo pia yako katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu na wa kupendeza kama unavyoyaona.
Hawa pia ni mafundi wakikokota mbao zao kwa ajili ya kwenda kujengea vibanda ndani ya viwanja hivyo....
Katika kazi hakuna kulemba, hata kina mama kibao wameweza kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo na kushirikiana na mafundi wa kiume katika ujenzi na ukarabati na wengi wao wamekuwa wakibeba zege na mchana viwanjani humo ni ilimradi tu mkono uende kinywani siku hizi wanawake pia hawachagui kazi jamani hivyo ukiwa na kazi yeyote usisite kumshirikisha mwanamama kwa kuhofia eti anaweza kukataa, ila isiwe ya ujambazi tu.
No comments:
Post a Comment