Ebwana huyu afande si kwamba anaigiza la hasha ni kweli yamemtokea hapa alikuwa katika mazoezi yanayoigiza kupanda mahala fulani iwe kwenye ndege ama pengine panapostahili kupandwa kwa kutumia kamba, lakini yaliyomtekea ni kama hivyo anavyoonekana suluali ikimvuka na asiju la kufanya kutokana na kuwa juu huku mikono yake ikimsaidia kupata balansi ili kufanikisha zoezi lake bila kuangua je afanyeje????.
Kazi ya Jeshi jamani haitaki mzaha wala lelemama kama wewe umezoea mambo ya home mboga saba kujisevia kwa mapozi ukienda jeshi uatakutana na kalinye kalinye na kasheshe kama hizi haina kulemba sahani ni chochote kitakachokuwa mbele yako, na ndiyo maana jamaa hawa wakimaliza mafunzo yao na wakarejea mitaani wanakuwa na hasira mbaya, ebwana eeh! usiwachokoze waha jamaa si unaona mwenyewe???
Wakati mwingine si kuigiza ila ni mchoko wa kweli unaweza kusinzia huku ukiwa umesimama wima. hebu mcheki huyu jamaa anavyopiga miayo.....huku wenzake wakiwa silisi katika paredi...
No comments:
Post a Comment