IGP AFUNGUA SEMINA YA SIKU MOJA YA WAHARIRI NA POLISI
Inspekta Jeneral wa Jeshi la polisi nchini, Said Mwema, akizungumza wakati akifungua rasmi mkutano wa Wahariri wa vyombo vya Habari na Polisi uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha Jamii kuhusu masuala ya Uchaguzi ujao. Jeshi la Polisi limewataka Wahariri wa vyombo hivyo na waandishi wa habari kwa ujumla kushirikiana katika kufikisha ujumbe na elimu tosha kwa Jamii kuhusu masuala ya uchaguzi ili uweze kuwa wa amani na utulivu. Pia alisema kuwa ili kufanikisha hilo na kuwafanya raia kuwa karibu na polisi Jeshi hilo lipo katika mchakato wa kuandaa Huduma 'Costomer Care' katika vituo vya Polisi ili kuweza kuondoa dhana ya raia kuwaogopa na kuwaona askari si watu wa kuweza kuwa karibu na raia. Katikati ni DCI Robert Manumba (kushoto) ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Kibanda. Aidha katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jeshi hilo limezindua kitabu cha Haki na Wajibu wa Mpiga Kura ambacho kiligaiwa kwa Wahariri waliohudhulia Semina hiyo ili kuweza kufikisha ujumbe sahihi kwa Jamii.
Hiki ndiyo kitabu cha Haki na Wajibu wa Mpiga Kura.
Hiki ndiyo kitabu cha Haki na Wajibu wa Mpiga Kura.
IGP Mwema na viongozi wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa katika mkutano huo.
Kaimu Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, akitoa mada na kuelezea yaliyomo katika Kitabu cha Haki na Wajibu wa Mpiga kura kilichochapishwa na jeshi hilo.
Mwezeshaji, Evod Mmanda, akitoa mada katika Semina hiyo..
Mwezeshaji, Evod Mmanda, akitoa mada katika Semina hiyo..
Kaimu Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, akiendelea kukichambua khicho.
Inspecka Jenerali wa Jeshi la Polisi, Said Mwema (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa vyombo vya Habari baada ya kufungua rasmi mkutano wa Polisi na Wahariri uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha Jamii kuhusu masuala ya Uchaguzi ujao.
Inspecka Jenerali wa Jeshi la Polisi, Said Mwema (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa vyombo vya Habari baada ya kufungua rasmi mkutano wa Polisi na Wahariri uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha Jamii kuhusu masuala ya Uchaguzi ujao.
IGP Mwema akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Meena. Katikati ni Kamishna wa Operesheni wa jeshi la Polisi, Paul Chagonja.
Wahariri wa vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mhariri wa Gazeti la Mtazanzania Deodatus Balile (kushoto) akiwa na baadhi ya wahariri wa vyombo vingine katika Semina hiyo.
Mhariri wa Gazeti la The African,Shermax (katikati) na Robert Komba (kushoto) wakiwa kwenye Mkutano huo.
Katika mkutano huo yalipitishwa maadhimio manne, ambayo ni pamoja na (1) Jeshi la Polisi na Vyombo vya Habari kuwa na ushirikiano endelevu.
(2) Pande hizo zote mbili kufanya kazi kwa pamoja dhidi ya uhalifu na kufuata maadili.
(3) Pande zote mbili kuonyesha Uzalendo kwa nchi yetu, pamoja na kukutana kila baada ya miezi 3 ili kujadili matokeo ya vikao vilivyopita na kuona faida zake.
No comments:
Post a Comment