Habari za Punde

*MAONYESHO YA WAKANDARASI YAFUNGULIWA LEO DAR

Naibu Waziri wa Miundombinu, Hezekiah Chibulunje (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi maonyesho ya siku mbili ya Wakandarasi, yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine ni viongozi wa Bodi ya Wandarasi.

Naibu Waziri wa Miundombinu, Hezekiah Chibulunje (kulia) akipokea kipeperushi na kusikiliza maelezo ya Mkurugenzi Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa, Aloyce Mwasuka, kuhusu kazi na huduma zinazotolewa na Shirika hilo, wakati wa maonyesho ya Wakandarasi yaliyoanza leo na kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

VIFAA HALISI VYA UMEME
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Cash Sale Store Ltd, inayojishughulisha na kuuza fifaa halisi na uhakika vya Umeme, Ali Jawad Jivraj-Bhimani (kushoto) akitoa maelezo kwa wateja na wakazi wa jijini Dar es Salaam, waliofika kwenye banda la maonyesho la Kampuni hiyo, wakati wa maonyesho ya siku mbili ya Wakandarasi yaliyoanza leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Kampuni hiyo, Hussein A. Tayabali. Kwa mahitaji yako ya vifaa halisi vya umeme wasiliana na Kampuni ya Cash Sale kwa namba:- 0767 295 815/ 0784 295 815 au 0767 786 125/ +971 508748327

Mkurugenzi Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa, Aloyce Mwasuka, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati walipotembelea kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya Wakandarasi yaliyoanza jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Waziri wa Miundombinu, Hezekiah Chibulunje, akisalimiana na Baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wakandarasi baada ya kuwasili kwenye ukumbi huo tayari kwa ufunguzi wa maonyesho hayo.

Meneja Masoko wa Dar Ceramica Centre 2001 Ltd, Frank Kombe, akitoa maelezo kwa mteja wake aliyefika katika banda lao wakati wa maonyesho hayo leo..Hapa ni Full Funiture za jikoni na bafuni.....

Banda la Dar Ceramica kwa nje......

Vifaa hivyo vilikuwapo kwa wingi ukumbini humo kama unavyoona hapa ni banda jingine pia likisheheni zagazaga kama hizi..

Huyu naye alikuwa akiwahi ndani na lijimtungi hili sijui ni la nini, wakandarasi bwana....









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.