Meneja Mkuu wa Uhusiano na mawasiliano kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers, Teddy Mapunda, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 35, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo tanzania, (TASWA) Boniface Wambura wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), leo mchana. Kulia ni mweka hazina wa TASWA, Tom Chilala na kushoto ni Katibu mkuu msaidizi wa TASWA, Amir Muhando , Serengeti imeamua kudhamini tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka anayechaguliwa na Taswa ambayo hutolewa kila mwaka na chama hicho ikiwa ni sehemu ya Kampuni hiyo kushiriki na kuchangia katika suala zima la michezo nchini.
Afya : Wadau washauri Bajeti mtazamo wa kijinsia kusaidia watoto Njiti
-
Na Deogratius Temba, Dar es salaam
Mtandao wa Haki ya afya ya uzazi umeshauri Serikali kutenga bajeti yenye
mtazamo wa Kijinsia katika sekta ya afya ili...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment