*HUYU DADA ALIYEBEBWA KATIKA PIKIPIKI ALIKUWA AKIONA AIBU AMA ANAOGOPA?Usafiri mwingine jamani utazani umelazimishwa kupanda, hebu mcheki huyu dada aliye katika pikipiki, sasa sijui alikuwa naumwa, anaogopa au anaona aibu kuonekana katika usafiri huo? ebwana eeh! mshkaji huyu alikuwa akikatiza katika mitaa ya Sinza Barabara ya Shekilango, kwa kweli hakujulikana chanzo cha abiria wake kufumba macho na ili asione anakokwenda, hali ya kuwa usafiri huo wenyewe wanasema Bodi ni mwili wako....
*BAJAJI YAPEWA BODI NA ROLI YENYEWE CHALI
Bajaji ikiwa imepinduka katikati ya barabara ya Shekilango eneo la Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam jana, baada ya kugongwa na Roli wakati ikijaribu kukatiza mbele yake katika njia panda. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.
*DAR BWA MVUA KIDOGO TU BALAA
Bajaji ikiwa imepinduka katikati ya barabara ya Shekilango eneo la Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam jana, baada ya kugongwa na Roli wakati ikijaribu kukatiza mbele yake katika njia panda. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.
Wasamaliawema wakisaidia kuiinua bajaji hiyo ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo, ambalo tayari kwa muda mchache tu ilikuwa ni balaa.
*DAR BWA MVUA KIDOGO TU BALAA
Hii ni barabara inayoelekea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ikiwa imejaa maji kutokana namvua iliyonyesha jana kwa dakika kadhaa tu, Na hii yote inasababishwa na Miundombinu mibovu katika maeneo yaliyo mengi ya Jiji la Dar es Salaam, ambayo imepitwa na wakati kwani mingine ni tangu enzi za mababu zetu na Wakoroni.
*HOTEL NDANI YA MJI WA KIHISTORIA BAGAMOYO
NANI MWENYE MAKOSA, ASKARI ANAYEMHOJI DEREVA KATIKATI YA BARABARA AU DEREVA ALIYEKUBALI KUHOJIWA KATIKATI YA BARABARA????
Hii ni Bonge ya Hoteli iliyopo katika mtaa fulani hivi mjini Bagamoyo ikiendelea kutoa huduma kwa wateja wake katika mazingira ambayo kwa kweli hayaridhishi kiafya, Any Way tuwaachie wahusika... ili kunusuru afya za wakazi na wapenzi wa hoteli hii...
NANI MWENYE MAKOSA, ASKARI ANAYEMHOJI DEREVA KATIKATI YA BARABARA AU DEREVA ALIYEKUBALI KUHOJIWA KATIKATI YA BARABARA????
Askari wa usalama barabarani, akimhoji dereva aliyefanya kosa katika barabara ya Bibi Titi jijini Dar es Salaam leo mchana, huku magari mengine yakipata taabu ya kuwakwepa ili kuendelea na safari, ama sijui Afande huyu aliogopa kukimbiwa na gari hii ama Dereva alikuwa mbabe hakutaka kufuata na kutii amri ya afande huyu, mie sijui mwiso wao ilikuwaje kwani kama unavyojua mjini hapa kila mtu na time yake na hasa nyakati za kazi......
No comments:
Post a Comment