Habari za Punde

*ONYESHO LA KHANGA PARTY YAKONGA MANGO GARDEN

Wasanii wanaounda kikundi cha 'Khanga Moja', wakionyesha umahiri wao wa kucheza miondoko ya taarab wakiwa na khanga moja tu, wasanii hao waliweza kuwachanganya mashabiki wa burudani waliokuwa wamejazana lukuki kwenye Ukumbi wa Manga Garden Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika onyesho la bendi ya Extra Bongo na Jahazi morden Taarab, ambapo walipanda jukwaani huku wakiwa wamevalia khanga moja tuuuuuu, na ndani wakionekana kuwa na zile Chunanilu wanazoziita Bikinaniliu zenye kamba tu, na kuwafanya mijidume iliyokuwapo ukumbini hapo kubaki ikidondokwa na mimate na kutunza kila muda bila kujali fedha anayotoa kwa madada hao, ama kweli Taarab imebadilika sidhani kama waasisi wa miondoko hii na hasa kina Bi kidude kama waliwahi kushuhudia mashabiki wao wa miondoko hii.....

Ilikuwa ni kumwaga radhi tu ukumbini hapo kila mmoja akionyesha uwezo wake wa kuzungusha mauno kwa staili zake na uwezo wake woooote.

Rapa wa kundi la Taarab la Jahazi Morden, Juma Said 'Domo Kaya' akiwachezesha madada hao wa Khanga Moja jukwaani.

Twende Saaaaaasaaaaaaa.......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.