*JAMAA AUZA MITEGO YA PANYA YA KICHINA HUKU AKIWA NA MFANO WA PANYA ALIYEKUFA.Mfanyabiashara wa mitego ya Panya ya Kichina, ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akitoa maelekezo ya jinsi ya kutega na kukamata panya kwa kutumia mtego wa plastiki wa Kichina, kama alivyonaswa na Sufianimafoto kwenye Mtaa wa Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Swali ni kwamba je mitego hiyo ya plastiki inauwezo wa kunasa panya kama huyu aliye 'Mdisplay' katika biashara yake kweli? au ndo changa la macho???? Panya kama hili si linaondoka na kijimtego chenyewe jamani.
*WADOSI WAKIJISEVIA MADAFU UFUKWENI
Hawa jamaa wao kwao kila siku ni sikukuu kama unavyowacheki hapa wakiwa kwenye Ufukwe wa bahari ya hindi eneo la Ocean Road, wakijisevia madafu kama walivyonaswa na Kamera ya Sufianimafoto jana Iujumaa mida ya saa saba mchana.
*MACHUNGA WAANZA KUVAMIA ENEO ZURI LA NJE YA OFISI ZA ZAIN MOROCCO.

Wafanyabiashara za mkononi, Machinga, wakiwa nje ya uzio wa Ofisi mpya za mtandao wa Simu za mkononi Zain, zilizopo Morocco, jijini Dar es Salaam, wakifanya biashara, hawa jamaa walipobughudhiwa baada ya mwezi tu utawakuta wamefika hadi mbele ya geti la ofisi hizo.
No comments:
Post a Comment