Habari za Punde

*MECHI YA UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA, SOUTH, MEXICO NGOMA DROO

Wachezaji wa Timu ya South Africa, wakitoka uwanjani kwa huzuni baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mexico, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia, mchezo uliochezwa leo jino. South ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 55, mfungaji akiwa ni mchezaji mahiri wa timu hiyo, Siphiwe Tshabalala.
Mexico walicharuka na kuliandama lango la South kila dakika huku mashambulizi yakiwa ni ya zamu kwa timu zote hadi dakika ya 79, Mexico walipofanikiwa kupata bao la kusawazisha kupiti kwa mchezaji wake, Rafael Marquez na kufanya timu hizo kutoka uwanjani zikiwa sawa kwa kufungana 1-1.
Hapa Bongo pia mashabiki wa soka walikuwa bize kufuatilia mchezo huo kupitia Luninga zao, huku ikionekana Wabongo wengi kuwa wazalendo kwa kuishangilia South Africa, jambo lililowafanya wengine kutawanyika baada ya kuona bao la kusawazisha likifungwa. Mchezo unaofuata ni kati ya Ufaransa na Uruguay, utakaochezwa mida ya saa 3.30 kwa saa za hapa nyumbani.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.