Kamanda wa Kikosi cha Madawa ya kulevya, Godfrey Nzowa, akionyesha mifuko iliyotumiwa na watuhumiwa, Diaka, raia wa Guinea na Abubakar, raia wa Nigeria, ikiwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine Kg 31, wakati wakiingia kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Juni 23 majira ya saa moja usiku. Nzowa alionyesha na mifuko hiyo iliyotumika kubebea madawa hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam leo mchana, ambapo alisema kuwa watu hao walikamatwa wakati walipofika uwanjani hapo wakitokea nchini Afrika ya Kusini na Ndege No, SA 199 na baada ya kukamatwa walidai kuwa wanatoka Ubalozi jambo ambalo liliwapa wasiwasi kidogo na kuwachukua muda kukata shauri la kuwasachi. Watu hao wapo mahabusu kwa upelelezi zaidi.
Askari akionyesha maandishi yaliyoandikwa katika mfuko huo, ambao hata wewe mdau unguona usingeweza kuutilia mashaka kiurahisi.
Askari wa kike akipanga vifurushi hivyo vya madawa yaliyokamatwa ili kuonyesha kwa waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment