Habari za Punde

*TANZANIA KUWA MWENYEJI WA RIADHA KWA VIJANA KANDA YA TANO AFRIKA




USAILI wa kuwapata vijana chini ya umri wa miaka 20, watakaoiwakilisha Tanzania katika mchezo wa Riadha Kanda ya Afrika umekamilika leo baada ya vijana hao kufanyiwa mchujo na kupatina wakali watakaounda kikosi cha Taifa.
Mchujo huo wa kuunda timu ya taifa ya riadha ya vijana chini ya umri wa miaka 20 itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Afrika kanda ya tano yametimua vumbi leo hii kwenye uwanja wa taifa jijini DSM.

Akizungumuza wakati wa mchujo huo katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania (RT) SULEIMAN NYAMBUI amesema Tanzania watakuwa wenyeji wa mashindano hayo na wao watayatumia kwa ajili ya kuunda timu ya taifa ya vijana ambayo baadhi ya wachezaji wake watashiriki katika michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika mjini NEW DELH nchini INDIA MWEZI OKTOBA mwaka huu.

Nao wanariadha waliobuka kidedea katika mbio za mita mia nne, mshindi wa kwanza MOHAM,ED CHARLES wa ARUSHA na mshindi wa pili JOSEPH MSILA wa DSM wamesema watafanya vyema katika mashindano hayo ya vijana ya Afrika kwani wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi.

Mashindano ya riadha ya kanda ya tano kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 yampepangwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 kwenye uwanja wa Taifa na yatashirikisha wanariadha kutoka nchi za MISRI, ETHIOPIA, ERITREA, KENYA, UNGANDA,BURUNDI,RWANDA na wenyeji TANZANIA. Habari na picha kwa hisani ya www.janejohn.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.