Habari za Punde

*MCHAKATO WA KUMPATA MWAKILISHI WA BSS MKOA WA DAR WAANZA COCOBEACH LEO

'Producer' wa Bongo Star Search BSS, Rod Gomez, akiwaandikisha majina vijana waliojitokeza kufanyiwa usaili ili kupata namba za kuingia kushiriki katika mchujo wa kutafuta mwakilishi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kinyang'anyiro cha Bongo Star Search, ambapo mchakato huo umenza leo kwa mkoa wa Dar baada ya kumaliza mbio hizo mikoani.


Vijana wakiwa katika foleni kubwa wakisubiri kupatiwa namba za kushiriki. Hata hivyo vijana hao walioonekana kuwa wengi kupita kiasi walilalamikia utaratibu walioandaliwa mahala hapo kuwa haukuwa wa kuridhisha kutokana na wao kufika mahala hapo kwenye Ufukwe wa Coco Beach saa 12 asubuhi wakati zoezi hilo lilianza midfa ya saa mbili.

Askari wa ulinzi wakijaribu kuwatuliza viajana waliokuwa wakisukumbana kuwahi foleni ili kupatiwa namba na kusababisha vurugu na mistari hiyo kuvurugika.

Hawa ni baadhi tu ya viajana waliobahatika kuwahi na kupatia namba wakiwa katika foleni ya kujiandikisha ili kushiriki zoezi hilo.



Mmoja kati ya washiri wa kike wa BSS aliyefanikiwa kuwai na kupata namba akielezea jinsi

Baadhi ya madada waliojitokeza kushiriki zoezi hilo walioonyesha kukata tamaa mapema baada ya kuchoka kusimama katika foleni wakipumzika chini ya mti.

Baadhi ya viajana waliojitokeza kufanyiwa usaili katika kinyang’anyiro cha kumsaka mkali wa Bongo Star Search, wakiwa chini ya miti ufukweni hapo wakati wakisubiri kujisajiri ili kujiunga na mchakato huo wakati wa zoezi hilo kwa mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika kwenye Ukumbi wa Coco Beach.

Nyomi la foleni mama nyoka...........









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.