Habari za Punde

*ZANTEL YATOA GARI LA DROO YA DONDOKA SAUZ

Mc wa hafla hiyo, Maulid Kitenge, akionyesha funguo za gari hilo wakati alipokuwa akitaja sifa na uzuri wa gari hilo la kisasa, wakati wa hafla hiyo ya kuchezesha Droo hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi za Zantel Msasani Jijini Dar es Salaam jana usiku na kurushwa Live kupitia Kituo cha ITV.

Ofisa Masoko wa Kampuni ya Magari ya Hyundai, Irene Kwimbere, akibonyeza kitufye cha Kompyuta kuchezesha droo ya kumtafuta mshindi wa gari aina ya Hyundai, katika Promosheni ya ‘Dondoka Sauz’ iliyokuwa ikichezesha na Kampuni ya Simu za mkononi ya Zantel, ambapo Corman Masaule (57) mkazi wa Hai Mkoani Kilimanjaro, aliibuka mshindi wa gari hilo katika droo hiyo iliyochezeshwa jana usiku Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao (katikati) ni Meneja Masoko wa Zantel, William Mpinga na Mshereheshaji wa hafla hiyo, Maulid Kitenge.


Wakipiga simu kwa mshindi huyo kumtambua na kumfahamisha juu ya ushindi huo wa gari.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.