Habari za Punde

*CHAMA CHA MADAKTARI (MAT) CHAADHIMISHA MIAKA 45

SERIKALI inampango wa kuboresha maslahi ya madkatari nchini ili kiwe kichocheo cha kuachana na mpango wa kutafuta kazi nje ya nchi ambako kunaaminika kuwa na
maslahi mazuri.

Hayo yalisema na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) uliofanyika jana jijini.

Profesa Mwakyusa alisema kuwa zaidi ya madakatari 100 wa Tanzania kwa sasa wanafanya kazi nje ya mipaka ya nchi, idadi ambayo ni kubwa kulinganisha na mahitaji ya nchi katika sekta hiyo.

Alisema kuwa pamoja na sekta ya Afya nchini kupata maendeleo makubwa, bado mahitaji ya huduma hiyo inahistajika kwa kiasi kikubwa kutokana na idadi ya madaktari hapa nchini.

Kwa mujibu wa Profesa Mwakyusa, Tanzania kwa sasa ina jumla ya madaktairi 6,000, idadi ambao ni kubwa kulinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema kuwa wakati Tanzania inapata Uhuru, kulikuwa na madaktari 21, wakati huo nchi ikiwa na idadi
ya watu Milioni 9.

“Kipindi kile, hakukuwa na Vyuo Vya Tiba, idadi hiyo iliongezeka miaka 20 baadaye ambapo tulikuwa na madakatari 500 Tanzania nzima ambapo jumla ya wanafunzi waliokuwa wanasomea taaluma hiyo ilikuwa 50, hii leo (jana), MAT
ikiwa inasheherekea miaka 45 tokea kuanzishwa kwake, tuna vyuo vikuu vya tiba vitano na jumla ya wanafuzni 500 wakisomea taaluma hiyo, tumepata maendeleo makubwa japo tunahitaji kuboresha zaidi,” alisema Profesa Mwakyusa.

Alisema kuwa serikali imeweka mikakati mbali mbali ili kuboresha sekta hiyo ikiwa moja na kutoa elimu zaidi na kuandaa miundombinu bora kwa wahitimu wake.

“Kwa sasa tuna maendeleo makubwa katika sekta hii na kuweza kufanya usajuaji wa moyo, kutibu magonjwa ya figo, kutibu saratani na magonjwa mengine ambayo awali ilibidi mgonjwa apelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu,” alisema.
Rais wa MAT, Dk.

Edith Ngirwamungu aliomba Serikali kutoa mazingira mazuri kwa madaktari ili kuwahamasisha wafanya kazi hapa nchini na kuepuka kukimbilia nje ya nchi.

Alisema kuwa madaktari wengi wanakumbana mazingira magumu mara wanapopangiwa vituo vya kazi na kuamua kutafuta njia nyingine ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha ikiwa pamoja na kwenda nje ya nchi.

“Daktari anapangiwa kazi huku akiwa hakuna nyumba na mshahara mdogo ambao hata hivyo kuupata unakuwa tabu, hali hiyo humfanya aachane na kazi za hapa nchini na kwenda kutafuta mashali zaidi nje ya nchi, ili kuepuka hilo, basi serikali iandae mazingira mazuri ambao yatawafanya waendelee kulitumikia taifa lao wakiwa hapa hapa nchini,” alisema Dk. Ngirwamungu.

Katika mkutano huo, MAT ikimpa tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa wa kuendeleza sekta ya afya nchini ikiwa pamoja na kujitolea kupima VVU
akiwa ma Mke wake, Mama Salma Kikwete na kushiriki katika promosheni ya vita dhidi ya Malaria (Zinduka).


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Brandina Nyoni, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa masuala ya Chumba cha Upasuaji wa Kampuni ya Anudha Ltd, Protas Soko, wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) katika mkutano wa 43 wa madaktari hao uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurgenzi wa Kampuni hiyo, Anurag Hassija.

Baadhi ya madaktari walioshiriki mkutano huo wa maadhimisho wakiwa kwenye chumba cha mkutano.

Sehemu ya maonyesho ya vifaa vya maabala.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.