Basi la Grazia lenye namba za usajali T 591 ADK linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es Salaam likiwa limeangula eneo la Mseke mkoani Iringa leo asubuhi. Abiria waliokuwamo katika basi hilo, wamenusurika kufa baada ya gari hilo kuanguka na gari la kubebea wagonjwa la Hospitali kuchelewa kufika eneo hilo la tukio ambalo lilikuwa ni kama Kilometa nane tu hadi kufika hospitalini hapo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya viongozi na Wakuu wa Wilaya walilazimika kukatisha msafara uliokuwa katika Ziara na kufika eneo la Tukio
Ajali hiyo ilitokea leo majira ya saa 3, asubihi katika eneo la Mseke mpakani mwa wilaya ya Iringa vijijini na Manispaa ya Iringa wakati basihilo likitokea wilayani Njombe kwenda jijini Dar es Salaam na wakati dereva akijaribu kulikwepa Lori bovu mbele usukani ulimshinda na basi hilo kuhama njia na kupinduka, alieleza mmoja kati ya abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo.
Baadhi ya viongozi na wananchi wakiwa eneo la Tukio.
Ajali hiyo ilitokea leo majira ya saa 3, asubihi katika eneo la Mseke mpakani mwa wilaya ya Iringa vijijini na Manispaa ya Iringa wakati basi
Baadhi ya viongozi na wananchi wakiwa eneo la Tukio.
Askari wa usalama Barabarani, wakisindikiza majeruhi katika gari la Mbunge, baada ya gari la kubebea wagonjwa kuchelewa kufika eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment