Habari za Punde

*ASASI ZILIZOFANYA VIZURI 2010 ZAPEWA TUZO

Mwendesha shughuli hiyo, ama msema chochote, Maria Sarungi, akiendesha hafla hiyo.
Rais wa 'The Foundation For Civil Society' , Dk. Stigmata Tenga (kulia) akimkabidhi na kumpongeza mshindi wa jumla wa Tuzo hizo, Katibu wa Asasi ya Young Women Christian Association ya mjini Mbeya, Mama Thabitha Bugali, wakati alipotangazwa na kukabidhiwa tuzo hiyo ya mshindi wa jumla wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za washindi wa Asasi zilizofanya vizuri mwaka 2010. Hafla hiyo ilifanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Asasi ya ‘Women Empowerment kwa ushirikiano na Wide Customer Outlet’.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Devota Likokola (kulia)akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Belita, Hellena Lutega kwa ajili ya asasi hiyo iliyofanya vizuri kwa kuwawezesha Wajasiliamali wadogo kwa mwaka 2010, wakati wa hafla fupi ya kutoa tuzo hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Oikocredit, Judy Ngarachu, akimkabidhi tuzo, Francis Mshana wa Asasi ya Mapambazuko ya Tabata Dar es Salaam, iliyofanya vizuri katika marejesho mwaka 2010.
Dk Stigmata Tenga, akizungumza wakati wa ufungaji wa hafla hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Devota Likokola, akimtunza msanii Mrisho Mpoto aliyekuwa akitoa burudani katika hafla hiyo.
Mrisho Mpoto na wanenguaji wa bendi yake, wakishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.








No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.