Habari za Punde

*DEREVA WA FUSO ATOLEWA NISHAI NA MDADA

Askari polisi akiamulia ugomvi wa Mwanadada huyu anayeonekana katikati, ambaye hakuweza kufahamika jina lake na dereva Fuso (kulia) ambaye anadaiwa kutaka kumkimbia bila kumlipa ujira wake kama ambavyo walikubaliana kabla ya kustarehe pamoja usiku wa kuamkia leo mjini Iringa. Mdada huyo amedai kuwa dereva huyo baada ya makubaliano walikwenda kupumzika katika nyumba ya wageni hadi asubuhi ambapo asubuhi dereva huyo alimuaga kuwa anakwenda kununua vocha nje, "Lakini kilichonishangaza ni pale nilipomuona amevaa kamili na kubeba kila kinachomuhusu nikashtuka na nilipotoka nje, nikamkuta akiingia kwenye gari lake na kumuwahi na nilipojaribu kumuomba pesa yangu kistaarabu aliniwakia sasa mie nifanye nini ameyataka mwenye ya kudhalilishwa" alisema mdada huyo.
Raia wakishuhudia tukio hilo...


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.