Habari za Punde

*MDAU NIMEIPENDA HII HAWA MADOGO WANAMAANISHA NINI?

Pichani ni askari wa kulinda usalama wa Shirika la Kimataifa la UN, wakati wakikatiza katika mitaa ya nchi fulani iliyokuwa imetawaliwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe, lakini wakati wakikatiza katika mtaa huu pembeni mwa gari walisimama watoto hawa na kupiga saruti kana kwamba walipangwa kufanya hivi.
Lakini hii inamaanisha watoto hawa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakiishi bila kuwa na amani mahala hapa na pindi tu walipowaona askari hawa walihisi amani imetua mahala hapo na kuwapigia saruti kumaanisha kuwaheshimu.
Na hii ni kwa sababu tu watoto hawa wamekuwa wakipishana na watu wa aina hii, milio ya mabimu na risasi mara kwa mara kiasi kwamba wameshazoea na kuiga kila kitu. 
Mtoto kama huyu usishangane ukamkuta ameshika mtutu eti naye yu mstari wa mbele tena anakuwa mbaya hasa kwani tayari anaweza kuwa ameshashuhudia baadhi ya nduguze ama wazazi wake wakifanyiwa unyama na kuuawa. "HILI NDILO TAIFA LA KESHO" tukeshe tukiomba amani iendelee kutawala Tanzania na ikiwezekana Afrika kwa ujumla kwa mambo kama haya yasikie tu kwa mwenzako usiombe yakutokee.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.