Habari za Punde

*MKALI WA HIP HOP, SHARAMA ATUA BONGO KUWASHIKA KWA PAMOJA NA TOTOO ZE BINGWA


Msanii mkali wa hip hop kutoka nchini Kenya, Ramadhan chambo, anayejulikana kwa jina la Sharama, amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa albamu yake ya 'vunja winga' hapa Tanzania kutokana na kuona ana mashabiki wengi wa miondoko yake hapa nchini ambao hawajapata kile wanachostahili kutoka kwake.

Akizungumza na Reporter wa Sufianimafoto, Sharama alisema “unajua nilikaa na kuona kuwa watanzania ni miongoni mwa mashabiki wangu na ninawapenda sana ndio maana nimeamua kuja kuwapa kile wanachokihitaji kutoka kwangu yaani burudani ya nguvu na hip hop ya ukweli”

Sharama ambaye kwa sasa amepiga kambi Bongo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka katika kundi la Ukoo wa Maumau kwa pamoja wamepiga kambi pale katika studio za Mzuka Record wakipata madini tofauti kutoka kwa mtu mzima Benjamini wa mambojambo.

Aidha Sharama aliwaomba mashabiki wake wote kuhudhuria kwa wingi pale Diamond jubilee siku ya tarehe 23/07 ambapo atakuwa akizindua albamu yake ya 'VUNJA WINGA'. 

“Ninachowaomba mashabiki wangu wa Tanzania ni kuibuka kwa wingi pale Diamond ili kuona nimewaandalia nini kama zawadi yao maana nina imani kuwa kuna kitu kikubwa mashabiki wangu wanakihitaji kutoka kwangu hivyo na mimi nitawapa siku hiyo”

Sharama pia ameishukuru taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Art In Tanzania' kwa kuwezesha mpango mzima wa uzinduzi wake.

Katika uzinduzi huo pia kutakuwa na uzinduzi wa albamu ya 'HAIELEWEKI' ya rapa mahiri wa bendi ya Akudo Impact Totoo ze Bingwa ambao nao kwa kiasi kikubwa umewezeshwa na kuletwa kwenu na Art In Tanzania.

Katika shoo hizi mbili za watu wazima kutakuwa na burudani ya kusindikiza kutoka kwa kundi zima la Ukoo flani Maumau, Abasi kutoka nchini Kenya na kutoka Tanzanina watakuwepo 20%, Benjamini wa mambojambo, Zolla D, Sana Asana Band na bendi ya Akudo Impact.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.