Habari za Punde

*TBL YATOA SH. MILIONI 34.5 KUSAIDIA MAJI VIJIJI 20 VYA IFAKARA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni y Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Maji Safi kwa  Afya Bora Ifakara (MSABI), Dk. Honorathy Urassa (kushoto), mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 34.5 za kusaidia awamu ya pili ya mradi huo. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ni Mshauri wa Miradi Maalumu wa TBL, Phocus Lasway (wa pili kulia) na Mhandisi wa MSABI, Naomi Mg'endo.
Huyu ni mmoja wa wananchi katika moja ya Vijiji vya nchini huko katika Kijiji cha Iwela Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa, akiwa katika harakati za kutafuta maji huku akiwa na watoto wake, jamani TBL jaribuni pia kufika katika maneo kama haya ili muweze kuwasaidia wananchi kupata huduma ya maji ambayo imetokea kuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi wa pembezoni mwa nchi lakini tatizo la maji si tu kwa wanakijiji bali pia hata katika majiji makubwa hata hapa Bongo kama huko Goba, Kimara na kwingineko.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.