Habari za Punde

*WASNII WA BONGO FLAVA KUZINDUA VIDEO YA MIAKA 50 YA UHURU

WASANII  wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava wako mbioni kuzindua Video ya wimbo wao wa Uhuru wa miaka 50.


Kiongozi wa Wasanii hao Said Fela, akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es Salaa le mchana, alisema kuwa, katika kusherehekea miaka hii 50 ya Uhuru, sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo zimeleta ajira kwa vijana. 

Si vibaya basi kwa kile kidogo walichopata wasanii hawa nao wakachangia kile wanachokipata kupitia sanaa zao katika kutoa shukrani kwa kutimiza miaka 50 ya Uhuru ikiwa ni sehemu ya kusherehekea.

"Sisi kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.

Kwa fikra zetu hii ni muhimu, na kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa burudani.?

Lakini jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika, kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.

Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.

Video hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36.

Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kutangaza uzinduzi huo wa Video ya Uhuru.

Mwenyekiti wa chama cha Wanamuziki,Tanzania Flava Unit, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa video ya miaka 50 ya uhuru wa sanaa ya Muziki. Video hiyo imerekodiwa na kampuni ya Visual Lab, yenye dakika zisizozidi nne ikiwa na lengo la kutowachosha  iliyowashirikisha wasanii zaidi ya 50 huku wengine walioingiza sauti wakiwa 36. Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.