Habari za Punde

*RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI ALI HASSAN MWINYI ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA CHUO KIKUU HURIA

  Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Samwel Malechela, akimtunuku Shahada ya Heshima Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi , wakati wa sherehe za Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Bungo Kibaha. Kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Samwel Malechela wakati wa mahafali hayo ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Bungo Kibaha.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Mhe. Samweli Malechela, akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa, Balozi wa Tanzania Nchini Urusi, Balozi Jaka Mwambi, katika Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Bungo Kibaha. kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.