Habari za Punde

*MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAENDELEO YA WANAWAKE ZANZIBAR (COWPZ)

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ) Balozi Amina Salum Ally, kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia Jumuiya hiyo, wakati wa  sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika  kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (wa pili kulia) akikata Keki maalumu iliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika  kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana. Wengine ni baadhi ya Viongozi  wa Jumuiya hiyo kutoka (kushoto) ni Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo, Vijana  Wanawakw na Watoto, Zainab Omary Juma, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif na (kulia) ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Balozi Amina Salum Ally.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipokea maandamano ya Wanawake na Vijana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipokea maandamano ya Wanawake na Vijana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza na Mkuu wa Kikundi cha Nuru ya Kisauni, Hamisa Maabad Ali, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe hizo.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, (wa pili kushoto) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif (kushoto) na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiliamali , Biubwa Said aliyekuwa akiwaelezea jinsi ya kuandaa Clips za Viazi, Mihogo na Tambi za Unga wa Dengu, wakati wa sherehe hizo.
 Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akijumuika kucheza  baadhi ya Kinamama waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ).
 baadhi ya Kinamama waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ).
 Keki ya Sherehe hizo...
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa zungumza waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake  Zanzibar (COWPZ).
Picha ya Pamoja baada ya sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.