Habari za Punde

*JAMBO LEO YAANZA VYEMA MICHUANO YA NSSF YAICHAPA TBC 2-1

Nahodha wa timu ya Jambo Leo, Mwinshehe, akimkabidhi zawadi ya majarida ya Gazeti la Jambo Leo, mgeni rasmi wa ufunguzi wa michuano ya NSSF, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, baada ya kuzindua rasmi michuano hiyo ya kombe la NSSF iliyoanza rasmi leo katika Viwanja vya TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kwa kuzikutanisha timu za Jambo Leo na TBC. Katika mchezo huo wa fungua dimba timu ya Jambo Leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TBC.

Wachezaji wa TBC na Jambo Leo wakichuana vikali katika mchezo huo kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe.
Katika michuano hiyo pia timu za Netiboli za IPP na Mwananchi, zilifungua dimba na katika mchezo huu, IPP wameibuka washindi kwa kuwwdhibu Mwananchi kwa mabao 16-12.
Kikosi cha timu ya TBC.
Kikosi cha timu ya Jambo Leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.