Habari za Punde

*EXTRA BONGO KUTAMBULISHWA WAPYA JUMANNE WIKI IJAYO

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki na mwimbaji wa bendi hiyo, Banza Stone, wakishambulia jukwaa katika moja ya maonyesho yao hivi karibuni.
*****************************************
*Kusikilizisha mpya na kutambulisha rapa mpya badala ya Ferguson
*Kusogeza uzinduzi wa albam yao kumalizia video za alba nzima

BENDI ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, wanatarajia kutambulisha wanamuziki wapya siku ya jumane na nyimbo zao mpya ‘Lisening Party’ na kutambulisha Rapa mpya wa bendi hiyo badala ya Ferguson aliyetimkia bendi ya Mashujaa.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com , Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kuwa wameamua  kusogeza uzinduzi huo kwa ajili ya kukamilisha kurekodi video za nyimbo za albam hiyo zilizosalia.
Choki,  alisema kuwa Albam hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 6 pamoja na Sebene moja la Shoo.
Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni Mtenda Akitendewa, uliotungwa na Ally Choki,  Falsafa ya Maisha, uliotungwa na Banza Stone, Neema uliotungwa na Athanas na Fisadi wa Mapenzi uliotungwa na Rogat Hega ‘Katapila, ambao unaendelea kumaliziwa kurekodiwa video yake.
Nyimbo nyingne ni pamoja na Mama Shuu wa Ally Choki na Bakutukaya, unaomaanisha (Wamekimbia) uliotungwa na Mnenguaji mahiri na kiongozi wa Jukwaa la wanenguaji wa bendi hiyo Super Nyamwela.
‘’Tunatarajia kufanya ‘Lisening Party’ siku ya Jumanne jioni katika Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori, ikiwa ni maalum kwa kuwasikilizisha waandishi wa habari pamoja na mashabiki wetu i watakaohudhuria kupata radha ya nyimbo zetu mpya.
Mbali na kuwasikilizisha nyimbo zetu mpya pia tutamtambulisha Rapa wetu mpya aliyeziba pengo la aliyekuwa Rapa wetu John Saulo ‘Ferguson’ aliyetimkia bendi ya Mashujaa, ambapo rapa wetu mpya , anayetambulika kwa jina la Frank Kabatano, aliyejinuga na bendi yetu akitokea bendi ya Tot Plus, ambaye tayari amekwisha tunga rap zake kadhaa ambazo atazitambulisha siku hiyo.
Hivyo tunaawaalika waandishi wa habari pamoja na wadau wetu na mashabiki wa muziki wa dansi waweze kufika katika ukumbi wa Meeda siku hiyo ili waweze kusikia vitu vipya kutoka kwa bendi yao pendwa ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’,  alisema Choki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.