Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAASISI YA WAKURUGENZI TANZANIA (IoDT)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati akizindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) alioizindua leo, kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT),  wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo, kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mussa Juma (wa pili kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) George Mkuchika na (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Pius Maneno.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Geoffrey Mmari kutoka Chuo cha Tumaini Dar es Salaam kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Ibrahim Mohamed Kaduma,  kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi  na baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali, baada ya kuzindua Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.