Habari za Punde

*BOB MAKANI AFARIKI DUNIA

Marehemu Bob Makani, enzi za uhai wake.
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema, ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bob Makani, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.

     Habari za kifo chake zimetolewa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye amesema kuwa, Bob Makani amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu, na mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

    Kufuatia kifo cha mwasisi huyo wa chama hicho, sasa Chadema wamekatisha ziara za kuimarisha uhai wa chama zilizokuwa zikiendelea katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.