Habari za Punde

*SHEREHE YA KUWAAGA WANAFUNZI WA MWAKA WA TATU WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YASOSHOLOJIA YA UDOM YAFANA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA UKUMBI WA VETA MJINI DODOMA

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Leph Gembe, (mbele) akiwasili ukumbini akiongozana na Mwenyekiti wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Misungwi, katika ukumbi wa veta uliopo Mkoani Dodoma katika Sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) jana.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Wa Pili Kushoto)Mh Leph Gembe akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao wamemaliza muda wao ambapo wa kwanza kushoto ni Mwalimu mlezi wa taasisi hiyo Bw. Jeremiah katika sherehe ya Kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanasoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiingia ukumbi kwa staili ya kucheza kwaito katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo dodoma mjini.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo mjini Dodoma jana.
Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Bi. Gaundensia Mwakemwa, akimvalisha kitambulisho Makamu Mwenyekiti Mpya, Bw. Mtono Juma,  kama ishara ya kukabidhi madaraka kwa viongozi wapya wa taasisi hiyo wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wa Sosholojia iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mwenyekiti mpya wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma, Bw. Edgar Kelvin, akimkabidhi zawadi mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Leph Gembe, ambaye pia alikua mgeni rasmi wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma.
Wadada safi kabisa wakiwa wamebeba keki tayari kwaajili ya kuikata.
Wawakilishi wa wanafunzi walioitwa mbele kwaajili ya kukata keki kutoka kushoto  ni Mwanafunzi Loyce Haule, (katikati) ni Shabani Kambi, na Beatrice Msami.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu na viongozi waliomaliza muda wao wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya Wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Leph Gembe, kama ishara ya kutambua majukumu yao kipindi wakiwa katika nafasi za uongozi.
Muda wa kujisevia ulikkuwa ka hivi....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.